1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM.Ripoti juu ya vita dhidi ya Hezbollah kutolewa leo

30 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC5s

Jopo la Israel lililoundwa kuchunguza vita vya dhidi ya Hezbollah leo linajiandaa kutoa ripoti yake ambayo inatarajiwa kuikosoa vikali serikali ya waziri mkuu Ehud Olmert.

Vyombo vya habari Israel vimefichua sehemu ya ripoti hiyo ambapo waziri mkuu Olmert amekosolewa kwa jinsi alivyoendesha vita na kufanya pupa ya kuanzisha mapambanao baada ya wapiganaji wa Hezbollah kuwateka nyara wanajeshi wawili wa Israel.

Ripoti hiyo pia inasemekana inamkosoa vikali waziri wa ulinzi Amir Perez na aliyekuwa mkuuwa jeshi Dan Halutz aliyejiuzulu wakati huo.