1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Waziri Steinmeir aitaka Israel kuendelea na juhudi za amani

7 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC47

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeir ameitaka Israel kuendelea na juhudi za kutafuta amani na wapalestina.

Katika mkutano wake huko Jerusalem na waziri wa mambo ya nje wa Israel Tzipi Livni, Steinmeir amesema kuendelea kwa juhudi hizo za amani mashariki ya Kati kutabakia kuwa suala muhimu katika sera za nje za Umoja wa Ulaya. Livni kwa upande wake amesema anapanga kwenda mjini Cairo baadae wiki hii kujadili juu ya kufufua mpango wa amani uliopendekezwa na nchi za kiarabu.