1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la serikali lauteka mji muhimu wa Qusseir

5 Juni 2013

Wanajeshi wa serikali ya Syria pamoja na Hisbollah wameukomboa mji muhimu Qusseir na kuwalisha hasara waasi.Ushindi huo umetangazwa huku Ufaransa na Uingereza zikisema jeshi la serikali limetumia gesi ya sumu ya sarin

https://p.dw.com/p/18jvP
Wanajeshi wa Syria wanasherehekea kukombolewa mji wa QusseirPicha: AFP/Getty Images

Mod:

       Wanajeshi wa serikali ya Syria na washirika wao wa Hisbollah wameukomboa mji muhimu wa mpakani wa Qusseir na kuwalisha hasara waasi waliopania tangu miaka miwili iliyopita kumpindua rais bashar al Assad.Ushindi huo umetangazwa katika wakati ambapo Ufaransa na Uingereza zinasema kuna ushidi  gesi ya sumu ya sarin imetumiwa na wanajeshi wa serikali ya Syria.Zaidi anasimulia Oummilkheir.

Waasi wanasema wameuhama mji wa Qussair unaopakana na Libnan baada ya wikmi mbili za mapigano makali yaliyoshuhudia kujiingiza kijeshi wanamgambo wa Hisbollah katika mzozo wa Syria.Mji wa Quseir  ulioko katika mkoa wa Homs ni muhimu tangu kwa seikali mpaka kwa waasi kwasababu ya njia panda zinazotumiwa kusafirishia silaha.Na kukombolewa mji huo uliokuwa ukidhibitiwa tangu zaidi ya mwaka mmoja na waasi inaangaliwa kuwa hatua muhimu na vikosi vya serikali katika juhudi zao za kuudhibiti mji wote wa Homs.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Hisbollah Al Manar,waasi wamekimbilia Dabaa na Buweida al Charquiya,vijiji viiwili vilivyoko kaskazini ya Quseir.

"Ndio tumeupoteza mji wa Quseir" amekiri mwanachama mmoja wa halmashauri ya mapainduzi ya Syria kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.

Hali hii inajiri mnamo siku ambapo wawaakilishi wa Umoja wa Mataifa,Marekani na Urusi wanapanga kukutana mjini Geneva kuzungumzia juhudi za kuitisha mkutanao wa amani kuhusu Syria na katika wakati ambapo Ufaransa na Uingereza wanaituhumu serikali ya rais Bashar al Assad kwa kutumia gesi ya sumu ya Sarin kataika mapigano hayo.

Alikuwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa Laurent Fabius aliyekuwa wa kwanza kuzungumzia madai hao aliposema:

O-Ton Laurent Fabius

"Kwa upande mmoja,wenzenu wa gazeti la Le Monde wanaostahiki kupongezwa wametupatia sampuli am,bazo tumezifanyia uchunguzi;kwa upande wa pili tumefuatilizia tukio jengine na kulichunguza sampuli zake:matokeo ya maabara ni dhahiri,kulikuwa na gesi ya Sarin.Suala kama tunaweza kusema nani walikuwa nyuma ya maatukio hayo:Katika kadhia hiyo ya pili hakuna shaka yoyote:serikali na washirika wake."

Na Uingereza nayo imesema wana ushahidi wa "kifisiolojia" unaobainisha gesi ya sumu ya sarin imetumiwa nchini Syria " na inaelekea imetumiwa na wanajeshi wa serikali".

Marekani inaendelea kusema ushahidi timamu inahitajika.

Mwandishi:Hamuidou Oummilkheir/Reuters/AP/AFP

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman