1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Syria ladhibiti barabara muhimu sasa

13 Mei 2013

Vikosi vya serikali ya Syria vinadhibiti barabara kuu inayounganisha mji wa Damascus na nchi jirani ya Jordan,ikiwa ni kusongambele kwa jeshi la serikali katika kampeni ya kuwaondoa waasi kutoka eneo muhimu la kusini.

https://p.dw.com/p/18Wlp
Syrian refugees watch the convoy of Babatunde Osotimehin (not pictured), Executive Director of the United Nations Population Fund (UNFPA), during his visit to the Zaatari refugee camp in the Jordanian city of Mafraq, near the border with Syria April 15, 2013. Osotimehin visited the Zaatari refugee camp in Jordan on Monday to underscore the urgent needs of women and youths affected by the conflict in Syria. REUTERS/Muhammad Hamed (JORDAN - Tags: CIVIL UNREST POLITICS SOCIETY CONFLICT)
Wakimbizi wakielekea nchi jirani ya JordanPicha: Reuters

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameishutumu Syria kwa kujaribu kuiingiza nchi yake katika mzozo wa Syria baada ya mashambulio mawili ya mabomu yaliyoua watu 46 katika mji wa mpakani

Waasi wanaopigana kuuondoa utawala wa rais Bashar al-Assad nchini Syria wanajaribu kupambana kutokea katika eneo la karibu ya mpaka na Jordan na kuingia upande wa jimbo la kusini la Daraa, katika kile kinachoonekana kama njia muafaka ya kuweza kuukamata mji mkuu Damascus.

Rebel fighters from the Al-Ezz bin Abdul Salam Brigade pose for picture as they attend a training session at an undisclosed location near the al-Turkman mountains, in Syria's northern Latakia province, on April 24, 2013. AFP / MIGUEL MEDINA (Photo credit should read MIGUEL MEDINA/AFP/Getty Images)
Wapiganaji wa jeshi la waasi nchini SyriaPicha: Miguel Medina/AFP/Getty Images

Waasi wapata pigo

Wiki chache zilizopita , waasi walipata mafanikio makubwa , lakini hivi karibuni wamepata pigo kutokana na mashambulio ya jeshi la serikali.

Majeshi ya serikali yameukamata mji wa Khirbet Ghazaleh siku ya Jumapili na waasi walikimbia kutoka eneo hilo, amesema Rami Abdul-Rahman, mkuu wa shirika la kuangalia haki za binadamu nchini Syria lenye makao yake makuu nchini Uingereza.

Majeshi ya serikali yalifungua tena barabara hiyo , na kurejesha uwezo wa barabara hiyo kupeleka vifaa baina ya Damascus na mji mkuu wa jimbo la Daraa ambao unaowaniwa na jeshi hilo.

Waasi wanadhibiti sehemu kubwa ya ndani ya nchi hasa upande wa kaskazini wa Syria , lakini maeneo hayo yako mbali kutoka mji mkuu kuliko mpaka na Jordan.

Russia's Foreign Minister Sergei Lavrov (R) and U.S. Secretary of State John Kerry talk during their meeting in Moscow, May 7, 2013. Russia and the United States agreed on Tuesday to try to arrange an international conference this month on ending the civil war in Syria, and said both sides in the conflict should take part. REUTERS/Mladen Antonov/Pool (RUSSIA - Tags: POLITICS CONFLICT)
John Kerry na mwenzake wa Urusi Sergei LawrowPicha: Reuters

Pendekezo la Urusi na Marekani kujadiliwa

Kundi kuu la upinzani nchini Syria la muungano wa kitaifa litakutana Mei 23 kujadili pendekezo la Urusi na Marekani la kufanyika mkutano wa kimataifa kuhusu suluhisho la kisiasa katika mzozo wa nchi hiyo.

Msemaji wa muungano huo Sonir Ahmed ameliambia shirika la habari la AFP kuwa mkutano huo utafanyika mjini Istanbul nchini Uturuki .

Pendekezo la Marekani na Urusi lililotangazwa mjini Moscow wiki iliyopita, linatoa wito wa kufanyika mkutano wa kimataifa kuyapa nguvu makubaliano yaliyofikiwa mwaka jana mjini Geneva kwa ajili ya suluhisho la kisiasa katika mzozo wa Syria.

Makubaliano ya Geneva yanatoa wito wa kusitishwa kwa matumizi ya nguvu na kuundwa kwa serikali ya mpito.

Waziri mkuu aonya

Wakati huo huo waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema jana kuwa Uturuki imewakamata watu tisa kuhusiana na mashambulio mawili ya mabomu yaliyotegwa katika gari ambayo yamesababisha vifo katika mji wa Reyhanli, lakini serikali ya Syria imekana kuhusika na shambulio hilo.

Relatives of Ahmet Uyan, 45, and Ahmet Ceyhan, 23, who were killed in yesterday's car bombings, mourn in the town of Reyhanli of Hatay province near the Turkish-Syrian border May 12, 2013. Turkey said on Sunday it believed fighters loyal to Syrian President Bashar al-Assad were behind twin car bombings that killed 46 people in a Turkish border town. Foreign Minister Ahmet Davutoglu said those involved in the bombings in Reyhanli on Saturday were thought also to have carried out an attack on the Syrian coastal town of Banias a week ago, in which fighters backing Assad were reported to have killed at least 62 people. Syria denied Turkish accusations on Sunday that it had a hand in twin car bombings. REUTERS/Umit Bektas (TURKEY - Tags: POLITICS CIVIL UNREST OBITUARY)
Shambulio la bomu dhidi ya UturukiPicha: Reuters

Tunapaswa kuwa watulivu zaidi. Uchokozi huu una lengo lake, ambao ni kuiingiza Uturuki katika vita vya Syria.

Serikali ya Uturuki imesema kuwa inawashikilia watuhumiwa wawili ambao wamekiri na kuishutumu Syria kwa kujaribu kuiingiza Uturuki katika mzozo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Turkey's Prime Minister Tayyip Erdogan listens during a news conference after the opening session of the fifth United Nations Alliance of Civilizations (UNAOC) Forum in Vienna February 27, 2013. REUTERS/Heinz-Peter Bader (AUSTRIA - Tags: POLITICS)
Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip ErdoganPicha: Reuters

Mashambulio hayo ni tukio baya kabisa katika kile ambacho wachunguzi wanaona kuwa ni kuendelea kutumbukia nchi za eneo hilo katika mzozo wa Syria ambao ulianza Machi mwaka 2011.

Akizungumza wakati wa ziara yake mjini Berlin waziri wa mambo ya kigeni wa Uturuki Ahmet Davutoglu ameyaita mashambulio hayo kuwa ni ukiukaji wa mstari wa Uturuki, na kuonya kuwa nchi yake inahaki ya kuchukua hatua yoyote inayostahili.

Mwandishi: Sekione Kitojo / ape / afpe

Mhariri:Yusuf Saumu