1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Uganda lawatia mbaroni washukiwa 20

22 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CfEP

Jeshi la Uganda limewakamata wanaume 20 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la waasi lenye maficho yake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Msemaji wa jeshi la Uganda, meja Felix Kulaije, amesema leo kwamba wanaume hao walikamatwa Jumanne iliyopita lakini serikali ikachelewesha kutangaza kukamatwa kwao ili kutoa nafasi uchunguzi ufanywe.

Meja Kulaije amesema stakabadhi zilizopatikana na wanaume hao 20 kutoka kambi ya wakimbizi ya Nakivale, zimedhihirisha kwamba wanashirikiana na kundi la waasi kutoka Rwanda lililo nchini Kongo.

Kundi hilo liliundwa na wanamgambo hatari wa kihutu wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994.

Washukiwa wote 20 wamekabibidhiwa polisi wa Uganda ili wafunguliwe mashtaka.