1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Uingereza laanza kuondoka katika mji wa Basra

3 Septemba 2007

Wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema kwamba vikosi vyake 550 vilivyoko eneo la Basra nchini Irak vitakabidhi mamlaka ya kituo hicho kwa wanajeshi wa Irak katika siku chache zijazo.

https://p.dw.com/p/CH8a
Kikosi cha Uingereza mjini Basra
Kikosi cha Uingereza mjini BasraPicha: AP

Vikosi vya Uingereza vilianza kuondoka kutoka mji wa Basra kusini mwa Irak kuanzia jana usiku katika hatua ya kukabidhi mamlaka kwa vikosi vya Irak huku Uingereza ikijitayarisha kuviondoa vikosi vyake kutoka nchini Irak. Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema kwamba maafisa wa Marekani walifahamishwa juu ya kuondoka kwa vikosi hivyo vya Uingereza kutoka mji wa Basra.

Wakati huo huo jemadari mwingine aliyestaafu wa jeshi la Uingereza amekosoa mkakati wa Marekani nchini Irak.

Katika mazungumzo na gazeti la jumapili la nchini Uingereza la SUNDAY MIRROR meja jenerali Tim Cross ameieleza sera ya Marekani nchini Irak kuwa imeshindwa kabisa kufaulu.

Meja jenerali Cross alikuwa afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Uingereza.