1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Ujerumani kuwajibika zaidi Afrika

20 Januari 2014

Uwezekano wa kuimarishwa shughuli za wanajeshi wa Ujerumani barani Afrika,mswada wa sheria kuhusu nishati mbadala na fujo za mashabiki wa dimba ni miongoni mwa mada magazetini

https://p.dw.com/p/1AtdF
Ndege ya jeshi la Ujerumani-Transall imetuwa katika uwanja wa ndege wa Mopti nchini MaliPicha: picture-alliance/dpa

Tuanzie na madai ya Ufaransa kutaka nchi za Umoja wa Ulaya ziwajibike zaidi katika shughuli za kulinda amani barani Afrika.Pendekezo hilo la Ufaransa inayoongoza opereshini za kulinda amani nchini Mali na kuanazia hivi karibuni katika jamhuri ya Afrika kati,limeitikwa vyema mjini Berlin.Gazeti la "Rhein-Neckar-" la mjini Heidelberg linaandika:"Waziri wa ulinzi Ursula von der Leyen atakapofika ziarani mjini Paris hii leo,atakabiliana na madai ya Ufaransa inayotaka kujua kama Ujerumani itaiunga mkono katika juhudi za kulinda amani barani Afrika.Hata kama juhudi hizo zinastahili sifa uhalali wake na ufanisi wake utapatikana ikiwa mkakati maalum utaandaliwa,na tena kutoka Umoja wa Mataifa na sio kokote kwengine.

Gazeti la "Bild" linahisi waziri wa ulinzi Ursula von der Leyen anakabiliwa na kishindo kikubwa.Gazeti linaendelea kuandika:"Mwezi mmoja baada ya kukabidhiwa wadhifa wake,waziri wa ulinzi Ursula von der Leyen anakumbana na ukweli wa hali ya mambo.Badala ya shule za chekechea na kazi za nusu siku kwa wanajeshi,sasa linazuka suala la jukumu halisi la jeshi la shirikisho-Bundeswehr:yaani -"Mapigano".Hakuna chengine kitakachowasaubiri wanajeshi pindi jukumu lao likiimarishwa barani Afrika,kwanza nchini Mali na baadae pia katika jamhuri ya Afrika Kati.Changamoto hizo zinamjilia mapema mno Ursula von der Leyen.Katika medani ya siasa ya nje bado hana maarifa.Na katika medani ya ndani anatiwqa kishibndo.Baadhi ya majenerali wameshaanza kumkosoa kichini chini.Na mawaziri wenzake wanamtia ila.Akifanikiwa kukaa kimya,atadhihirisha anachokifanya ni kwa masilahi ya wanajeshi kwa hivyo na kishindo hicho pia ataweza kukimudu."

Nishati mbadala haiepukiki

Mada yetu ya pili magazetini inahusu mageuzi katika sekta ya nishati.Gazeti la "Badische Neueste Nachrichten " linaandika:"Sigmar Gabriel anajaribu kisichowezekana.Anataka kuyanusuru mageuzi katika sekta ya nishati kwa kuzuwia kwanza kuanzishwa mageuzi hayo,anataka kuinusuru nishati mbadala kwa kuamua itumike hatua kwa hatua.Hatua kali zikichukuliwa huenda zikasababisha malalamiko miongoni mwa wahusika.Lakini maarifa ya miaka ya nyuma yameonyesha,marekebisho yanahitajika.Bila ya mipango,juhudi za kupanuliwa mradi wa nishati mbadala zinatishia kuleta madhara kila upande kuanzia mtandaoa mpaka kufikia akwa wanunuzi.

Siemens Windenergie Windkraftanlage
Mtambo wa nishati ya upepo ulitengenezwa na kampuni ya Ujerumani-SiemensPicha: picture-alliance/dpa

Matumizi ya nguvu viwanjani

Mada yetu ya mwisho magazetini inahusu fujo za mashabiki wa dimba nje ya aviwanja vya mpira.Gazeti la mjini Cologne-"Stadt Anzeiger" linaandika:"Ilikuwa bahati tu kwamba hakuna aliyefariki dunia jumamosi katika mtaa mmoja mashuhuri wa Cologne.Kwamba matumizi ya nguvu yasiyokuwa na maana yoyote yamejiri mnamo siku hiyo ya jumamosi, mchana kweupe,si jambo linalokubalika.Mwendesha mashtaka anaabidi awaandame na kuwafikisha mahakamani haraka waliofanya fujo hizo.Lakini hata mashabiki wenyewe wanawajibika kuwatenga watu wenye kutumia nguvu kama hao.

Fußballrandale St. Pauli und Hansa Rostock
Machafuko kati ya makundi ya wafanyafujo toka timu za St.Pauli na Hansa RostockPicha: picture-alliance/dpa

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri. Mohammed Abdul-Rahman