1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi lafanya mapinduzi Niger

Kabogo Grace Patricia19 Februari 2010

Baada ya mapinduzi hayo, utawala wa kijeshi ukaivunja serikali

https://p.dw.com/p/M5N8
Rais wa Niger aliyepinduliwa, Mamadou Tandja.Picha: picture alliance / dpa

Kikosi cha jeshi nchini Niger kimethibitisha kufanya mapinduzi nchini humo na kutangaza kuwa kimeivunja serikali ya nchi hiyo. Tangu jana Rais wa Niger Mamadou Tandja na baraza lake la mawaziri wanazuiliwa na wanajeshi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Niamey. Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi-ECOWAS, zimelaani mapinduzi hayo ya kijeshi.

Mvutano wa kisiasa umekuwa ukiendelea nchini humo baada ya Rais Tandja mwezi Agosti mwaka uliopita kulivunja bunge na mahakama ya kikatiba akishinikiza katiba ya nchi hiyo ifanyiwe mabadiliko yatakayomuwezesha kuendelea kuwepo madarakani kinyume na katiba, hatua iliyokosolewa ndani na nje ya nchi hiyo.