1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jimbo la Marekani New Jersey kuondosha adhabu ya kifo

14 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CbUz

WASHINGTON: Bunge la jimbo la New Jersey nchini Marekani limepiga kura kuondosha adhabu ya kifo.Kuambatana na sheria mpya,uhalifu mkubwa kabisa utaadhibiwa kifungo cha maisha,bila ya kuwepo uwezekano wa kuachiliwa huru mapema.Kwa hivyo,New Jersey karibuni,litakuwa jimbo la 14 kutokuwa na adhabu ya kifo.

Mahakama Kuu ya Marekani katika mwaka 1976, iliruhusu upya adhabu ya kifo.New Jersey ni jimbo la kwanza kuondosha adhabu ya kifo tangu wakati huo.