1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jimbo la Turkana lafurahia kupatikana kwa maji

Josephat Nyiro Charo4 Septemba 2014

Waturkana wafurahia kugunduliwa kwa hifadhi ya maji jimboni mwao yatakayoyafanya maisha yao kuwa rahisi kwani wamekuwa wakihangaika kutokana na uhaba wa maji kwa muda mrefu.

https://p.dw.com/p/1D6Hr
Turkana Kenia
Picha: Andrew Wasike

Huku ulimwengu ukiadhimisha wiki ya maji duniani, wakaazi wa jimbo la Turkana nchini Kenya wanalo jambo la kufurahia. Ni wakati kama huu mwaka uliopita ambapo watafiti waligundua hifadhi kubwa ya maji yenye mita za ujazo bilioni 250. Maji yanayoweza kutosheleza mahitaji ya nchi nzima kwa muda wa zaidi ya miaka 50. Na kama mwandishi wetu Alfred Kiti kutoka Nairobi anavyotufahamisha, wakaazi wa eneo hilo sasa wamepata sababu ya kutabasamu baada ya serikali kuanza kuwachimbia visima.

Mwandishi: Alfred Kiti

Mhariri: Iddi Ismail Sessanga