1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG: Ahadi kusaidia kifedha Afrika zitimizwe

1 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBw9

Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair ameyahimiza madola tajiri,kutimiza ahadi zilizotolewa, kusaidia kifedha nchi za Kiafrika.Amesema,kukosa kufanya hivyo,kutahatarisha maendeleo ya demokrasia na juhudi za kupiga vita umasikini barani Afrika.Akizungumza mjini Johannesburg, katika hotuba yake yenye ujumbe maalum,Blair vile vile alisema,viongozi wa Kiafrika wapaswa kuwa na msimamo mkali kuhusu serikali za kiimla, akimaanisha Sudan na Zimbabwe.Hapo awali alikutana na rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela.Ziara hii ya Tony Blair barani Afrika,imeshampeleka Libya na Sierra Leone pia. Waziri Mkuu wa Uingereza Blair anaondoka madarakani tarehe 27 mwezi huu.