1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG : Kiongozi wa utawala wa ubaguzi afariki

1 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCxH

Rais wa zamani wa utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Pieter Willem Botha amefariki dunia nyumbani kwake katika eneo la Western Cape akiwa na umri wa miaka 90.

Botha aliepachikwa jina la Mamba Mkubwa kutokana na sera zake kale za ukandamizaji ameiongoza Afrika Kusini chini ya utawala wa wazungu wachache kati ya mwaka 1978 na mwaka 1989. Amekaidi kulaaniwa kimataifa kwa mfumo wa ubaguzi wa rangi nchini humo ulioambatana na umwagaji damu mkubwa.

Hata baada ya kustaafu kwake aliendelea kuwa na msimao huo wa ufedhuli kwa kugoma kufika mbele ya tume ya ukweli ya nchi hiyo ambayo ilimhusisha na ukiukaji wa haki za binaadamu.