1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG: Mandela azindua kundi la kutenzua matatizo

18 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhP

Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini,Nelson Mandela hii leo ametimiza miaka 89.Afrika ya Kusini imeadhimisha siku ya kuzaliwa kwake,kwa kumsifu na kumpongeza kiongozi huyo mashuhuri aliepinga utawala wa ubaguzi wa rangi.Mandela binafsi ameiadhimisha siku yake ya kuzaliwa,kwa kuzindua kundi jipya la kimataifa kwa azma ya kusaidia kutenzua matatizo ya kimataifa kwa njia ya upatanisho na majadiliano sawa na vile utawala wa ubaguzi wa rangi ulivyomalizwa.