1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG: Mkuu wa polisi wa zamani ahukumiwa kifungo cha nje

18 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYE

Aliekuwa waziri wa sheria na utulivu wa Afrika Kusini,Adriaan Vlok na polisi wanne,wamehukumiwa kifungo cha nje kwa makosa ya kupanga njama ya kutaka kumuuwa mwanaharakati aliepinga utawala wa ubaguzi wa rangi.Washtakiwa hao watano walikiri makosa ya kutaka kumuua Mchungaji Frank Chikane, kwa kutia sumu katika chupi yake.

Kesi hiyo inatazamwa kama mtihani wa kesi za maafisa wa enzi ya ubaguzi wa rangi,ambao hawakusamehewa na Tume ya Ukweli na Upatanisho nchini humo.