1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG: Ndege ya abiria yarudishwa

6 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5Z

Ndege ya abiria iliyokuwa imeondoka uwanja wa ndege wa mjini Cape Town nchini AfrikaKusini imelazimishwa irudi, baada ya abiria mmoja katika ndege hiyo kuwatisha marubani.

Msemaji wa shirika la ndege la Kulula.com amesema ndege hiyo ilirudi katika uwanja wa kimataifa mjini Cape Town nusu saa baada ya kuondoka kwa sababu ya kitisho cha abiria huyo. Abiria huyo pamoja na washirika wake wametiwa mbaroni na polisi.

Hakuna abiria yeyote miongoni mwa abiria 159 waliokuwa ndani ya ndege hiyo aliyejeruhiwa na shughuli katika uwanja wa ndege wa Cape Town hazikutatizwa.