1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Johannesburg. Wachimba migodi waanza kuokolewa.

4 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ii

Waokoaji wameanza operesheni leo Alhamis ya kuwatoa wachimba migodi 3,200 kutoka chini ya ardhi zaidi ya saa 15 baada ya kukwama ,nchini Afrika kusini.

Kiasi cha wafanyakazi hao 150 wamekwishatolewa nje ya mgodi huo wa Elandsrand, kusini magharibi ya mji wa Johannesburg ilipofika saa nane na nusu usiku wa leo lakini wafanyakazi wote hawatarajiwi kuokolewa katika muda wa saa kumi zijazo.

Msemaji wa mgodi wa Harmony Gold Amelia Soares amesema kuwa wafanyakazi wa mgodi huo wamekwama kiasi cha mita 2,200 chini ya ardhi baada ya waya wa umeme unaoendesha lift kukatika. Mgodi huo uko katika eneo la Carletonville karibu na Johannesburg.