1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNSBERG:Mgomo wa wafanyikazi Afrika Kusini

13 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsB

Wafanyikazi wa umma nchini Afrika Kusini wanafanya mgomo wa wiki mbili huku mgomo ukitarajiwa kupanuka zaidi hii leo baada ya vyama vingine vya wafanyikazi kuwataka wanachama wao wakiwemo polisi kujiunga kwenye mgomo huo kuwaunga mkono wafanyikazi hao.

Wafanyikazi wa umma wanataka kuongezewa mshahara.

Mgomo huu ndio mkubwa kabisa tangu kumalizika mfumo wa ubaguzi wa rangi miaka 13 iliyopita. Mgomo huo tayari umetatiza shughuli nyingi zikiwemo shule, zahanati na huduma za umma.

Shughuli za bandari kuu ya mjini Durban pia zimesimamishwa.

Serikali ya rais Thabo Mbeki imeongeza mshahara wa wafanyikazi wa umma kwa asilimia 7.25 lakini vyama vya wafanyikazi hao vinatetea asilimia 10.

Vyama hivyo vimeishutumu serikali kwa kuweka kipaumbele zaidi katika uchumi wa soko badala ya kuwasaidia wananchi wengi walio maskini.