1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Joseph Kabila ameshinda duru ya pili ya uchaguzi wa rais katika jamahuri ya kidemokrasi ya Kongo

16 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsC

Kinshasa:

Jumuia ya kimataifa imewatolea mwito wanasiasa wote katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo wayakubali matokeo ya uchaguzi yanayodhibitisha ushindi wa rais Joseph Kabila.Taarifa ya pamoja iliyotiwa saini na Umoja wa mataifa,Umoja wa Ulaya na benki kuu ya dunia imewasihi zaidi watetezi wa kiti cha urais wajizuwie na aina yoyote ya uchokozi.Kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliyotangazwa hadi sasa Joseph Kabila amejikingia asili mia 58 za kura,na mshindani wake makamo wa rais Jean Pierre Bemba amejipatia asili mia 42.Kufuatia malalamiko ya Jean Pierre Bemba matokeo hayo yatabidi kwanza yaidhinishwe na mahakama kuu ya jamahuri ya nchi hiyo.Itafaa akusema hapa kwamba mnamo wiki za hivi karibuni,machafuko kati ya kambi mbili zilizokua zikiania kiti cha rais,yaligharimu maisha ya watu wasiopungua wanne.