1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za amani mashariki ya kati

Hamidou, Oumilkher2 Juni 2008

Waziri mkuu wa Israel aakutana na kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina licha ya mpango wa Israel wa kujenga mitaa ya wayahudi mashariki ya Jerusalem

https://p.dw.com/p/EBLi
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani ziarani Mashariki ya katiPicha: picture-alliance / dpa / AP / Montage DW



Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinemeier alikua ziarani Ramallah hii leo na kuzungumza na kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas.


Ziara ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani nchini Israel na katika ukingo wa magharibi inafanyika katika wakati ambapo Israel imetangaza mpango wa kujenga mitaa miwili itakayokua na nyumba 884 za wahamiaji wa kiyahudi katika eneo la mashariki la Jerusalem.


Mwishoni mwa mazungumzo pamoja na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinemeier,kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas amesema tunanukuu:"itakua shida kufikia makubaliano ya amani pamoja na Israel ikiwa mitaa ya wahamiaji wa kiyahudi itaendelea kujengwa katika ardhi za wapalastina."Mwisho wa kumnukluu Mahmoud Abbas.


Kiongozi huyo wa utawala wa ndani wa Palastina ameishukuru Ujerumani kwa juhudi zake za upatanishi kati ya Israel na Hisbollah ili waachiwe huru wafungwa wa pande hizo mbili,pakiwepo uwezekano wa kuachiliwa pia wafungwa wa kipalastina.


 Mahmoud Abbas ameishukuru pia Ujerumani kwa kuusaidia utawala wa ndani wa Palastina,kiuchumi,na katika sekta ya usalama na sheria pia.


Serikali kuu ya Ujerumani inapanga kuitisha mkutano wa kimataifa June 24 ijayo mjini Berlin kwa lengo la kuimarisha uchumi, na mfumo wa usalama na sheria katika ardhi za wapalastina.


"Tunabidi tuharakishe  ikiwa tunatilia maanani mpango wa kufikia mswaada wa amani hadi ifikapo mwezi November ujao" amesema waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani akimaanisha uchaguzi wa rais wa Marekani.


Kabla ya Ramallah,waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani alikua ziarani mjini Tel Aviv ambako aliuzungumza na waziri mwenzake  Tzipi Livni na waziri wa ulinzi wa Israel Ehud Barak.


 Baada ya mazungumzo pamoja na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani,kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas alikwenda Jerusalem ya mashariki kwa mazungumzo tete pamoja na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert.


Mazungumzo hayo yanafanyika muda mfupi pia kabla ya waziri mkuu wa Israel kwenda Marekani mdhamini mkubwa wa utaratibu wa amani uliofufuliwa November mwaka jana huko Annapolis.


"Ujenzi wa makaazi ya wayahudi na hatima ya wafungwa ni miongoni mwa madaa kuu tutakazozizungumzia" amesema Mahmoud Abbas mbele ya waandishi habari mjini Ramallah, kabla ya mazungumzo hayo kuanza.


Chama cha itikadi kali cha Hamas kinayataja mazungumzo hayo kua ni "kiini macho."Hamas wanamshutumu Mahmoud Abbas kuhalalisha ujenzi wa makaazi mepya ya wahayudi kwa kukubali kuzungumza na Ehud Olmert.


Mwishoni mwa mazungumzo hayo,waziri mkuu Ehud Olmert atakwenda Washington baadae hii leo kwa kile kinachoangaliwa kua "ziara ya mwisho ya kiongozi huyo wa serikali ya Israel anaezongwa na miito ya kumtaka ajiuzulu.