1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za kusaka ufumbuzi wa mzozo wa mashariki ya kati zashika kasi

14 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Fm

Tel Aviv:

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice ameanza hii leo ziara ya siku kadhaa katika eneo la mashariki ya kati.Mara baada ya kuwasili mjini Tel Aviv,mkuu huyo wa diplomasia ya Marekani,ameionya Israel isiendelee kunyakua ardhi zaidi za waarabu,akisema hali hiyo itavuruga imani katika juhudi za kusaka ufumbuzi wa madola mawili na kuundwa dola la wapalastina.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice aliyepangiwa kuzungumza na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmer na rais wa utawala wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas ,ili kuandaa mkutano wa mwezio ujao kuhusu amani ya mashariki ya kati,amesema haamini kama ziara yake hii itasaidia kufikiwa makubaliano.Hata hivyo wajumbe wa tume za waisrael na Palastina wameanza kuratibu kile waziri Rice alichokiita “waraka wa pamoja kuhusu mada muhimu.”Mbali na ziara yake mijini Jerusalem na Ramallah,waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani amerpangiwa pia kufika ziarani nchini Misri na Jordan.