1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za kuwapatanisha wapalastina

Hamidou, Oumilkher9 Oktoba 2008

Misri imeingia njiani kuwaleta pamoja ndugu wanaohasimiana wa kipalastina

https://p.dw.com/p/FX76
Waziri mkuu wa utawala wa ndani wa Palastina Salam FayyadPicha: AP


Wawakilishi wa makundi mawili ya wapalastina wanaohasimiana,Fatah na Hamas watakutana october 25 ijayo mjini Cairo Misri kwa mazungumzo ya kuunda serikali ya mpito itakayo yaridhisha makundi yote.Ripoti hiyo imetangazwa na afisa mmoja wa ngazi ya juu wa Hamas.



„Fatah na Hamas watakutana Cairo October 25 ijayo ,chini ya upatanishi wa Misri,ili kusawazisha hitilafu zao juu ya namna ya kufikia suluhu na kumaliza mfarakano kati ya wapalastina“,amesema hayo Mahmoud Al-Zahar,mwanasiasa mwenye shawishi mkubwa katika chama cha Hamas.


Mahmoud Al Zahar alishiriki katika majadiliano ya jana mjini Cairo pamoja na mkuu wa idara ya upelelezi ya Misri,jenerali Omar Suleiman,ambae mnamo wiki za hivi karibuni amekua na mazungumzo pamoja na makundi dazeni kadhaa ya wapalastina,likiwemo lile la Fatah la rais wa utawala wa ndani Mahmoud Abbas.


Misri inajaribu kuyaleta pamoja makundi yanayohasimiana ili kumaliza mzozano uliosababishwa na uamuzi wa Hamas wa kunyakuwa madaraza Gaza mwezi June mwaka jana.



Fatah inahisi mazungumzo ya Cairo yanabidi yafungue njia ya kuundwa serikali ya ridhaa itakaysokua na jukumu la kuandaa uchaguzi wa bunge na rais katika ardhi za wapalastina.


Hamas,wanaodhibiti bunge la Palastina lililochaguliwa january mwaka 2006 kwa kipindi cha miaka minne,wanashikilia uchaguzi wa rais tuu ndio unaostahiki kuitishwa.Wameshasema hawatomtambua Mahmoud Abbas kama rais wa utawala wa ndani,baada ya january nane mwakani,wakihoji mhula wake wa miaka minne utamalizika tarehe hiyo.


Jana lakini afisa mmoja wa chama hicho ,Khalil al-Haya amesema chama chao kiko tayari kulileta „suala la uchaguzi katika meza ya majadiliano.“


„Tumekubaliana kimsingi pamoja na viongozi wa Misri kuhusu masuala yanayobidi kujadiliwa tutakapokutana october 25 ijayo“ amesema Mahmoud Al Zahar na kuongeza tunanukuu:miongoni mwa masuala hayo ni pamoja na kundwa serikali ya ridhaa ya taifa na kufanyiwa marekebisho vikosi vya usalama kwa msaada wa wataalam wa kiarabu.“Mwisho wa kumnukuu.


Kwa mujibu wa bwana Mahmoud Al Zahar serikali ya ridhaa ya taifa itawashirikisha pia wanasiasa wa kujitegemea na wasomi.


Mkutano wa October 25 mjini Cairo utafuatiwa na mazungumzo ya makundi 13 ya wapalastina huko huko Cairo.Lengo muhimu ni kurejesha umoja wa kijeografia na kisiasa uliokuepo kabla ya June mwaka jana.


Salam Fayyad,mtaalam wa kiuchumi aliyechaguliwa na Mahmoud Abbas kua waziri mkuu,baada ya Hamas kunyakua madaraka Gaza,ametoa mwito kwa upande wake paundwe serikali isiyoelemea upande wowote wa kisiasa itakayokua na uwezo wa kuungwa mkono na jumuia ya kimataifa hadi chaguzi zitakapaoitishwa.



►◄