1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jukwaa la kimataifa la vyombo vya habari Bonn

3 Juni 2009

"Media Forum duniani"

https://p.dw.com/p/I2iC
Maripota kazini-LebanonPicha: dpa

Kuanzia leo hadi ijumaa, wanakutana mjini Bonn,Ujerumani, kubadilishana maarifa na ujuzi waandishi habari,mabingwa wa fani ya mawasiliano ya data ulimwenguni,magwiji wa mtandano na wamilikaji vyombo vya habari .

Kikao hiki kinajulikana kwa jina la "Global Media Forum"-Jukwaa la vyombo vya habari na mawasiliano ulimwenguni.

Jukwaa hili mjini Bonn, limewaalika waakilishi wa vyombo vya habari kutoka kila pembe ya dunia kutoka fani ya siasa,utamaduni,uchumi na sayansi.

Hii ni mara ya pili Jukwaa hili la "GLOBAL MEDIA FORUM " linafamnyika mjini Bonn.

Jukwaa la mara hii linafanyika chini ya mada: "Kuzuwia migogoro katika enzi ya vymbo vya habari vya aina mbali mbali":

Deutsche Welle inajiangalia kuwa ni sauti ya wajerumani katika kutetea haki za binadamu.Na sasa haki za binadamu zinakiukwa mno tangu katika migogoro ya kimataifa,vita vya kienyeji na hata katika vita vya kikabila.Ni wazi kwahivyo, jwa Deutsche Welle kujishughulisha na jinsi ya kuzuwia ugomvi wa aina hiyo kutokea.

Ulimwengu wa vyombo vya habari na mawasiliano, umepanuka nao mnamo miaka michache iliopita kupitia uvumbuzi wa mtandao,ufundi mpya , "Facebook" au hata "Twittler" na ndio maana Jukwaa hili la pili la "MEDIA FORUM" mjini Bonn, linafanyika kwa jina la " Kuzuwia ugomvi katika enzi hizi za aina mbali mbali ya zana za mawasiliano."

Bw.Ralf Nolting akiwa mkurugenzi wa Shirika la utoaji huduma katika sekta ya voymbo vya habari,amechangia mno kuandaa ratiba ya jukwaa hili la siku tatu hapa Bonn.Anasema:

"Kuna mikutano ya kutosha inayozungumzia maswali jumla ya kisiasa.Pia kuna mikutano ya kutosha juu ya vyombo vya habari.Sisi tunaitisdha mkutano unaounganisha sekta hizo m,bili.Hii maana yake: Upande mmoja tuna watu na mashirika yanayojishughulisha n amaswali motomoto yanayoendesha dunia yetu:hawa ni wanasiasa,wataalamu wa sayansi na mashirika yasio ya kiserikali (NGOS) .

Kwa upande wapili,tuna wale wanaojisghulisha sekta ya uenezaji habari,mfano wa waandishi-habari,wamilikaji vyombo vya habari kibiashara na pia wataalamu wa sayansi wanaochambua athari za vyombo vya habari kwa watu.Pia mafundi wa zana za uenezaji habari wanaoshika kichwa na kujiuliza :jinsi gani vyombo vya habari vinaendelea kukua na kupanuka."

Deutsche Welle katika mchango wake kwenye jukwaa hili mwaka huu halikupanga tafrija nyingi kwenye ukum bi wa mkutano.Zitakuwapo bila shaka, lakini imepanga zaidi warsha ndogo-ndogo n a mijadala.Katika hafla kama hizo mchango wa wajumbe unawezekana sio tu kutolewa, bali unatakiwa hasa.Kwa jumla, "Jukwaa hili la voymbo vya habari duniani"-global Media Forum, imepanga jumla ya hafla 50 mbali mbali.Na mipango hiyo imewavutia wajumbe wengi mkutanoni kama anavyoeleza zaidi Bw.Ralf Nolting wa DW:

"Tumepokea jumla ya taarifa kutoka wajumbe 1.200 wanaotaka kushiriki.Kawaida mtu huchukulia 10% watajitoa,lakini tunatazamia hadi wajumbe 900 watachangia.Na kwa mwaka huu wa msukosuko wa fedha na uchumi , hayo ni matokeo mazuri sana."

Jukwaa hili linafunguliwa leo kwa hotuba ya na Bw.Howard Rheingold,mmmoja kati ya wavumbuzi wa mtandao wa Internet.Rheingold akifanya taftishi kwa miaka mingi jinsi ufundi wa kimamboleo wa mawasiliano unavyoweza kuwa.Alivutiwa sana jinsi gani vymbo vya mawasiliano vya Mobile na vya mtandao, vinavyowawezesha wanadamu tena kwa kasi kubwa kuwasiliana.Uwezekano huo mfano ule wa SMS, uliongoza 2001 kumuangusha madarakani Rais wa Philipine,Joseph Estrada.Hapa Bonn, Bwe.Rheingold, anazungumzia leo vipi chombo kama hicho kinaweza kuchangia kuzuwia ugomvi na migogoro.

Mtayarishaji: Ramadhan Ali

Mhariri: M.Abdul-Rahman