1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Julai 2, siku aliyozaliwa marehemu Patrice Lumumba

2 Julai 2015

Miaka 50 iliopita Lumumba ambaye kama angekuwa hai , leo angetimiza miaka 90, aliiongoza Congo kujipatia Uhuru kutoka kwa Ubeligiji, lakini muda mfupi baadae akauwawa kwa idhini ya Ubeligiji na Marekani

https://p.dw.com/p/1Frcj
Patrice Lumumba Kongo Belgien Brüssel Haft
Waziri mkuu wa kwanza wa Congo, Patrice emery Lumumba.Picha: Getty Images

Leo ni siku aliyozaliwa waziri mkuu wa kwanza wa Congo , nchi inayojulikana sasa kama Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, marehemu Patrice Emery Lumumba. Miaka 50 iliopita Lumumba ambaye kama angekuwa hai , leo angetimiza miaka 90, aliiongoza Congo kujipatia Uhuru kutoka kwa Ubeligiji, lakini muda mfupi baadae akauwawa kwa idhini ya Ubeligiji na Marekani.

Sawa na kina mahatma ghandi wa India dhidi ya Ukoloni wa Uingereza , Stephen Biko dhidi ya makaburu nchini Afrika Kusini na Ernesto Che Guevara aliyepigana dhidi ya Udikteta nchini Cuba, Patrice Lumumba aliyezaliwa 1925 ambaye pindi angekuwa hai leo angetimia umri wa miaka 90, aliiongoza Congo kunyakulia uhuru 1961. Lumumba alikuwa kitisho kwa mkoloni Uibeligiji na na akakamtwa 1959 na kuteswa lakini akaachiwa huru kutokana na uasi uliozuka nchi nzima.

Lumumba alishinda kiti cha bunge katika uchaguzi wa kwanza mwezi Mei 1960 akawa waziri mkuu wa kwanza wa Congo. Katika hotuba yake iliyowasisimua wengi wakati wa sherehe za Uhuru Juni 30 ,1960, akijibu ile ya Mfalme Baudouin wa Ubeligiji aliyesifu kile alichokiita mafanikio ya ustaarabu ya ufalme wa Ubeliji na walowezi wake katika Congo, Lumumba akipingana na kauli hiyo alisema ,"Tumepigana vita hivi vya haki na heshima kumaliza utumwa uliotrushusha hadhi, kulazimisha ukandamizaji wa aibu wa utawala wa kikoloni. Mlitufanyia visa vya kejeli ,matusi na vipigo kila asubuhi, mchana na usikun kwa sababu tu tulikuwa ni weusi. " Mfalme akataka kuondoka mara moja lakini wapambe wakamrai abakie.

Hata hivyo ushindi wa Lumbumba haukudumu muda mrefu, hotuba yake dhidi ya mkoloni mbele ya mfalme ikaiudhi Ubeligiji, ambayo haikutegemea Congo ingejitawala kwa kuwa ikidaidika kutokana na utajiri mkubwac wa mali asili wa taifa hilo.

Waziri mkuu mpya akaandamwa na makundi ya kisiasa nje na ndani. Sehemu ya jeshi iliotumiwa na vibaraka wa Ubeligiji, ikaasi na kutokana na hali hiyo kukazuka uvumi wa visa vya ubakaji dhidi ya wanawake wa Kizungu. Jeshi la Ubeligiji likapata sababu na kuivamia Congo Julai 10 . siku moja baadae Mkoa wa kusini wa Katanga wenye utajiri wa mkubwa wa maadini yakiwemo ya almasi na shaba ukatangaza kujitenga. Akitengwa na nchi za magharibi na kupewa mgongo na Umoja wa Mataifa, Lumumba akaigeukia Urusi.

Kutokana na hayo ikawa sawa na kusaini adhabu ya kifo chake mwenyewe. Mpango wa kum,uuwa ukaandaliwa na Shirika la Ujasusi na Marekani na Idara ya usalama ya Ubeligiji, kama serikali ya ubeligiji ilivoykiri binafsi 2002. Patrice lu8mumba aliuwawa Januari 17 ,1961 huko Elizabethville inayojulikana leo kama Katanga. “Mshirika wake mmoja wa kisiasa wa zamani alimtaja Lumumba kuwa sawa na Nyota iliotanda mbiguni na baadae kutoweka.”Congo imebakia kuwa dola miaka 50 baadae pamoja na misukosuko ilioendelea kuikumba.

Dikteta Mobutu Sese Seko alitawala kwa karibu miaka 40 baada ya kifo cha Lumumba kufuatia mapinduzi yake ya kijeshi hadi 1997. Mfuasi wa zamani wa Lumumba Laurent desire kabila akamuangusha Mobutu na kutwaa madaraka Januari 2001, miaka 40 baada ya Lumumba.

Vita vya kuwania utajiri wa mali asili ya Congo vinaendelea na katika hili, hata baadhi mataifa ya Umoja wa Ulaya mikono yao pia si safi . Pamoja na hayo yote, ingawa Lumumba hakuishi muda mrefu baada ya kuikomboa nchi yake, Jina lake bado ni mwenge unaoendelea kuwaka sio tu nchini Congo, bali Afrika kwa jumla.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman, KNA

Mhariri:Iddi Ssessanga