1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jumuiya ya nchi za kiarabu yataka jenerali Sleiman achaguliwe rais wa Lebanon

6 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Ckvu

Mawaziri wa mashauri ya kigeni wa jumuiya ya nchi za kiarabu, ikiwemo Syria, wamekubaliana kwa pamoja kumuunga mkono kamanda mkuu wa jeshi la Lebanon, jenerali Michel Suleiman, achaguliwe rais wa Lebanon.

Baada ya Saudi Arabia na Qatar kumshinikiza mjumbe wa Syria katika mkutano wa mjini Cairo, Walid al Moallem, mawaziri wa jumuiya ya nchi za kiarabu wameidhinisha taarifa ya pamoja inayovitaka vyama vinavyohasimiana nchini Lebanon vimchague jenerali Sleiman na kumaliza tofauti zao za kisiasa.