1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jumuiya ya Ulaya yatafuta njia ya kuyawezesha mataifa masikini kupata dawa kwa bei nafuu.

Sekione Kitojo21 Julai 2007

Taasisi pekee ya umoja wa Ulaya ambayo wajumbe wake wanachaguliwa moja kwa moja na wapigakura inavutana na serikali za mataifa hayo 27 wanachama wa umoja huo kuhusiana na hatua ambayo inalengo la kuhakikisha kuwa mataifa masikini yanakuwa na uwezo wa kupata madawa muhimu.

https://p.dw.com/p/CHk4

Katika mwaka 2003, umoja wa Ulaya ulisaidia upatikanaji wa makubaliano ya muda ya msamaha kutoka katika shirika la biashara la dunia WTO kuhusu haki miliki ya mali za kitaaluma, ambayo inajulikana kwa kifupi TRIPS. Msamaha huo ulitayarishwa ili kuruhusu mataifa masikini ambayo yanakosa uwezo wa kutengeneza madawa ambayo yangetumika katika ulinzi wa dharura wa afya ya jamii kwa kuagiza madawa rahisi yenye kibali maalum cha kulindwa na kutoweza kuigwa chini ya leseni maalum.

Miaka minne baadaye , watendaji wa umoja wa Ulaya , ambao ni tume ya umoja wa Ulaya pamoja na serikali kadha za umoja huo zinajiwinda ili kuidhinisha itifaki ya kubadilisha TRIPS ili kuufanya msamaha huo kuwa wakudumu. Wakikutana Julai 17, hata hivyo , kamati ya bunge ya umoja wa Ulaya inayohusika na biashara ya kimataifa iliamua kuchelewesha kutoa kauli yake ya kuidhinisha kwasababu haijaridhika kuwa umoja huo unafanya vya kutosha kuimarisha usambazaji wa madawa muhimu kwa wanaoyahitaji.

Ikiwa hadi sasa hakuna nchi hata moja masikini ambayo imekwisha omba msamaha huo, wajumbe wa bunge la Ulaya wanalalamika kuwa imethibitika kuwa mpango huo haueleweki kwa urahisi na hauwezi kufanyakazi. Julai 19, hata hivyo, shirika la WTO lilitangaza kuwa Rwanda imekuwa nchi ya kwanza kusema kuwa inania ya kutumia msamaha huo.

Mbunge wa chama cha kisoshalist kutoka Ufaransa Kader Arif amesema kuwa kamata ya biashara itahitaji utaratibu wa dhati kutoka kwa tume hiyo pamoja na serikali za mataifa ya umoja wa Ulaya , kuwa mataifa hayo yatahusika moja kwa moja katika kutafuta suluhisho jipya.

Ikiwa katika njia moja pamoja na matarajio ya watu, umoja wa Ulaya unapaswa kulenga kuwa kiongozi wa dunia katika juhudi za kutengeneza dawa ambazo zinaweza kununuliwa na watu wa kila kipato duniani kote, ameongeza . Hii lakini ni zaidi ya kuidhinisha itifaki ya kimataifa. Hili ni suala ambalo linahusika na siasa na matatizo ya kiutu katika kiwango kikubwa, jibu lake likiwa hata hivyo linahitaji nia ya dhati ya kisiasa.

Tunaitaka tume kujitokeza na hatua mbadala za dharura zenye lengo la kusaidia mataifa yanayoendelea kuweza kutengeneza uwezo wao binafsi wa kutengeneza madawa.

Akizungumza mjini Strasbourg, Ufaransa, Julai 11, Olli Rehn mjumbe wa halmashauri ya umoja wa Ulaya , ameyataka makampuni ya madawa kutumia mfumo unaojulikana kama wa kuwekea masharti bei, ili kuuza madawa kwa bei nafuu katika mataifa masikini kuliko katika mataifa tajiri. Baadhi ya wabunge wanadai kuwa matarajio yake kuwa makampuni yatakubali kupoteza faida, kwa njia hii inaonekana kuwa tume hiyo haikuwa makini juu ya kutafuta suluhisho la uhaba wa madawa nafuu kwa ajili ya magonjwa makuu yanayouwa kama vile AIDS.

Alexandra Heumber, mwanaharakati wa kampeni inayofanywa na kundi linalopigania hali ya kiutu Medecins Sans Frontieres MSF, amelalamika kuwa Olli Rehn ameweza tu kutoa mifano juu ya vipi umoja wa Ulaya unatoa fedha kwa ajili ya utafiti kwa ajili ya uwezekano wa matibabu mapya ya magonjwa, kuliko kushughulikia suala la jinsi gani mali za kitaaluma zinazolindwa zimechangia katika kuzuwia watu masikini kuweza kupata dawa kwa bei nafuu.