1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabila aashiria ushindi nchini DRC

3 Desemba 2011

Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yanaonyesha kuwa rais wa hivi sasa, Joseph Kabila, anaongoza dhidi ya mpinzani wake Etienne Tshisekedi.

https://p.dw.com/p/13Lt6
epa03018091 A Congolese voter stamps her finger print after voting for the presidential election at a polling station in the capital Kinshasa, the Democratic Republic of Congo, 28 November 2011. Voting began despite concern of delay and violence while may voters complained of missing their names on the voters' list, late opening of polling stations and missing ballot papers. Seventy eight-year-old top opposition leader Etienne Tshisekedi of Democracy and Social Progress (UDPS) and Vital Kamerhe, a former UDPS member, are among many others who are challenging incumbent Joseph Kabila in the country's second election since the end of a bloody civil war in 2003. Election-related violence has already broken out in parts of the country and many predict that post-election violence is almost certain, if incumbent president declares victory. EPA/DAI KUROKAWA +++(c) dpa - Bildfunk+++
Zoezi la kupiga kura DRCPicha: picture-alliance/dpa

Kwa mujibu wa matokeo yaliotangazwa jana, karibu asilimia 15 ya kura zilizohesabiwa zinaonesha kuwa Kabila anaongoza kwa zaidi ya kura milioni 1.52 - hiyo ni takriban kura asilimia 52.

Tshisekedi ambae ni miongoni mwa wagombea 11, ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 997,074 au asilimia 34. Rais wa Tume ya Uchaguzi, Daniel Ngoy Mulunda ametoa matokeo hayo ya awali, ikiwa ni siku nne baada ya kufanyika uchaguzi, jumatatu iliyopita.

Waandalizi wa uchaguzi, wametoa mapema baadhi ya matokeo hayo ili kukabili tarakimu za bandia zinazosambazwa kwa kutumia ujumbe wa simu za mkononi na katika tovuti. Habari hizo za uongo zimesababisha mivutano.

Wadakuzi wa mtandao walisambaza matokeo ya bandia kwenye tovuti ya afisa wa Tume ya Uchaguzi, ambayo yameonyesha kuwa Tshisekedi anaongoza kwa kiasi kikubwa. Msemaji wa Tume ya Uchaguzi, Matthieu Mpita, alinukuliwa akisema kuwa wadakuzi wameingia katika tovuti yao.

epa03016707 A photo made available 27 November 2011 shows an injured supporter of the Union for Democracy and Social Progress (UDPS) being carried away by colleagues after clashes with police and army forces in Kinshasa, Democratic Republic of Congo 26 November 2011. The supporters were waiting for the main opposition leader, Etienne Tshisekedi, who was not allowed to hold a rally in town. Presidential and parliamentary elections will be held in on 28 November 2011. EPA/Yannick Tylle +++(c) dpa - Bildfunk+++
Vurugu za za uchaguziPicha: picture-alliance/dpa

Awali shirika la haki za binadamu "Human Rights Watch" lenye makao yake makuu nchini Marekani, lilisema kuwa kiasi ya watu 18 wameuawa kabla ya uchaguzi huo kuanza katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Wengi wao walipigwa risasi na wanajeshi kutoka kikosi cha walinzi wa Rais Joseph Kabila.

Matokeo kamili yanategemewa kutolewa Desemba 6 na baadae lazima yathibitishwe na Mahakama Kuu.

Mwandishi: Sudi Mnette/RTRE
Mhariri: Martin,Prema