1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabila alaumu majeshi ya nje kwa vurugu za DRC

30 Juni 2012

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo amelaumu waasi na wapiganaji kutoka nje ya taifa lake kwa kuendeleza machafuko katika maeneo ya mashariki mwa Kongo.

https://p.dw.com/p/15OVi
kabila.jpg **FILE** President Joseph Kabila smiles during a meeting with former heads of state in Kinshasa, Congo in this Saturday, Nov. 4, 2006 file photo. Kabila appeared to have an insurmountable lead Tuesday, Nov. 14, 2006, in Congo's runoff election with nearly all the votes counted. (AP Photo/Schalk van Zuydam, FILE)
Rais wa DRC Joseph KabilaPicha: AP Photo

Hata hivyo Rwanda imekwisha kanusha madai kwamba inalisaida jeshi lililoasi la waasi wa zamani wenye asili ya Kitutsi ambao kwa hivi sasa wanajulikana kama M23 ambao waliijuinga na jeshi la DRC na baadae kuasi.

Akizungumza katika televisheni ya serikali ,rais Kabila alisema sherehe za uhuru wa Kongo, zinakugubikwa na vitendo vya uasi vinavyofanywa na wapiganaji wa waasi pamoja na wapiganaji kutoka nje ya taifa hilo.

Amesema vitendo hivyo vimeleta machafuko katika eneo la Kivu ya Kaskazini na kusababisha maelfu ya raia kuteseka na kutokuwa na usalama. Kutokana na hali hiyo rais Kabila amesema kuimarisha usalama katika eneo hilo ni suala la kipaumbele, na kwa namna yeyote, kwa gharama yeyote watalilinda taifa na kulifanya kuwa nchi ya amani.

Democratic Republic of Congo's President, Joseph Kabila, right, and Rwanda's President, Paul Kagame, shake hands before a meeting in Abuja, Nigeria, friday June 25, 2004. Kagame and Kabila are here to attend a peace talk for Congo. (AP Photo/Saurabh Das)
Joseph Kabila na Paul Kagame nchini NigeriaPicha: AP

Katika kufanikisha azma yake kiongozi huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo amesema jitihada za kijeshi, kisiasa na kidiplomasia zinazofanyika sasa zitaendelea katika kutatua tatizo hilo. Rwanda imekuwa ikishutumiwa kwa kuunga mkono uasi nchini humo lakini Kabila hakulitaja taifa hilo katika hotuba yake.

Kiongozi wa waasi katika eneo la machafuko Bosco Ntaganda, mbabe wa kivita anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita kwa tuhuma za uhalifu wa kivita. Jumanne iliyopita ilitoa ripoti iliyosema kuwa afisa wa ngazi ya juu wa ulinzi nchini Rwanda kwa wadhfa wake amekuwa akiwasadia waasi kwa kuwapa silaha na misaada mingine yakiwemo mafunzo.

Majina ya maafisa hao yaliotajwa ni Waziri wa Ulinzi wa Rwanda, James Kabarebe, na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Charles Kayonga. Hata hivyo Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikawabo amesema ripoti hiyo inahitaji uchunguzi.

Mwandishi: Sudi Mnette/AFP
Mhariri: Abdu Mtulya