1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabila atangazwa rasmi mshindi wa uchaguzi Kongo

Tsuma, Carolyne/ZPR17 Desemba 2011

Mahakama Kuu katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo imeidhinisha tangazo la tume ya uchaguzi nchini humo kuwa rais Joseph Kabila amechaguliwa tena katika uchaguzi mkuu wa tarehe 28 mwezi uliopita.

https://p.dw.com/p/13Udz
**FILE** President Joseph Kabila smiles during a meeting with former heads of state in Kinshasa, Congo in this Saturday, Nov. 4, 2006 file photo. Kabila appeared to have an insurmountable lead Tuesday, Nov. 14, 2006, in Congo's runoff election with nearly all the votes counted. (AP Photo/Schalk van Zuydam, FILE)
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPicha: AP

Majaji wa mahakama hiyo iliyo katika mji mkuu Kinshasa wameyakataa matakwa ya upinzani kuwa matokeo hayo yafutiliwe mbali. Mawakili wa mgombea aliyeibuka wa tatu katika kinyanganyiro hicho cha urais na spika wa zamani Vitalis Kamerhe, waliondoka mahakamani humo wakiueleza uamuzi huo wa mahakama kuwa "kinaya ya haki".
Mahakama hiyo iliamua kuwa Kabila ameshinda uchaguzi huo kwa asilimia 48.95 dhidi ya mpinzani wake mkuu Etienne Tshisekedi aliyepata asilimia 32.33. Wiki iliyopita Tshisekedi aliyakataa matokeo yaliyotangazwa hapo awali na alijitangaza kuwa rais wa taifa hilo, huku akitoa wito wa kuhifadhi utulivu.