1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Hali ya usalama ni ngumu nchini Afghanistan

17 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqs

Kiongozi wa EUPOL,tume ya Umoja wa Ulaya kutoa mafunzo kwa polisi nchini Afghanistan,Friederich Eichele amesema,ana matumani mema kuhusu ufanisi wa kikosi cha polisi wa Kiafghanistan.Eichele amekiri kuwa hali ya usalama ni ngumu nchini Afghanistan.Wakati huo huo akaongezea kuwa uzoefu wa tume zingine umezingatiwa na anaamini kuwa wamejitayarisha vyema kwa hali hiyo ngumu ya usalama.