1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul: Inadaiwa helikopta ya Kimarekani imedunguliwa huko Afghanistan

18 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCR4

Majeshi ya muungano yanayoongozwa na Marekani katika Afghanistan yamesema moja ya helikopta zao imeanguka katika eneo la kusini mashariki ya nchi hiyo. Katika taarifa, muungano huo umesema ulianzisha msako na shughuli ya kuiokoa helikopa hiyo na watu waliokuwemo ndani yake baada ya rubani kuripoti kwamba aligundua kuna hitilafu katika injini ya helikopta hiyo. Waasi wa Taliban wanadai wameidungua helikopta hiyo kwa kutumia roketi.