1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Kharzai apendekeza mazungumzo ya amani na Taliban

29 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWg

Rais wa Afghnasitan Hamid Kharzai amependekeza mazungumzo ya amani na wapiganaji wa kundi la Taliban kufuatia mwaka ulioshuhudia umwagikaji mwingi wa damu nchini humo tangu wanamgambo wa Taliban walipoangushwa kutoka madarakani manmo mwaka wa 2001.

Zaidi ya watu 4,000 wakimwemo raia 170 wa kigeni waliuwawa kwenye mapigano mnamo mwaka jana, mwaka ulioshuhudia ongezeko kubwa la mashambulio ya mabomu yaliyofanywa na washambuliaji wa kujitolea mhanga maisha.

Rais Karzai ametoa pendekezo hilo alipokuwa akihutubia umati wa wati kwenye sherehe ya kidini mjini Kabul katika siku takatifu zaidi katika kalenda ya madhehebu ya Shia, lakini halikutaja kundi la Taliban.

Rais Karzai amesema anawaombea wale wanaopanga njama dhidi ya Afghanistan, akizungumzia Pakistan ambako wanamgambo wa Tasliban na washirika wao wa kiislamu wana maficho yao.