1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Kiongozi mmoja wa Taliban auawa nchini Afghanistan

13 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2W

Maafisa wa serikali ya Afghanistan wamesema kiongozi mmoja mkuu wa kundi la wanamgambo wa Taliban Mullah Dadullah ameuawa katika eneo la kusini mwa nchi hiyo.

Idara ya habari ya wizara ya mambo ya ndani imesema Mullah Dadullah aliuawa pamoja na ndugu yake wakati wa harakati za kijeshi katika mkoa wa Helmand.

Mullah Dadullah, ambaye ni kiguru, ni maarufu kwa kuandaa mikakati ya kijeshi ya kundi la Taliban na alikuwa rafiki yake mkubwa kiongozi mkuu wa kundi hilo Mullah Muhammed Omar aliye mafichoni.