1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Kiongozi wa Taliban auwawa.

24 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgU

Duru katika jeshi la Marekani nchini Afghanistan zinasema kuwa kamanda wa ngazi ya juu wa Taliban , anayetambulika kuwa yuko karibu na Osama bin laden , ameuwawa katika shambulio la anga. Taliban hata hivyo , limekanusha madai hayo na kusisitiza kuwa Mullah Akhtar Mohammed Osmani yu hai.

Duru hizo za Marekani zimesema kuwa Osmani aliuwawa siku ya Jumanne katika shambulio la anga la majeshi ya Marekani wakati akisafiri kwa gari katika eneo la jangwa katika jimbo la kusini la Helmand.

Watu wengine wawili aliokuwa nao pia wameuwawa.

Osmani ni kiongozi wa ngazi ya juu wa Taliban ambaye majeshi ya muungano yamedai kuua ama kuteka nyara tangu majeshi ya Marekani kuivamia Afghanistan.