1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Kituo cha polisi kimeshambuliwa kwa makosa

12 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsS

Helikopta ya Marekani kwa makosa imeshambulia kituo cha polisi cha Afghanistan na kuua polisi 7 na kuwajeruhi wengine 5.Kwa mujibu wa polisi walionusurika,helikopta hiyo ilishambulia,licha ya polisi kujaribu kuizuia na kupiga makelele. Maafisa wa Afghanistan wamesema,kosa hilo lilitokea,wakati vikosi vya majeshi ya ushirikiano yalikuwa yakishambulia washukiwa ugaidi katika wilaya ya Nangarhar.Amesema,tukio hilo linafanyiwa uchunguzi.