1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Majeshi ya muungano yadai kumuua mshirika wake Osama.

23 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgi

Jeshi la Marekani nchini Afghanistan limesema kuwa majeshi ya muungano yamemuua mshirika wa karibu wa Osama bin Laden. Jeshi limesema kuwa Mullah Akhtar Mohammed Osman pamoja na wapiganaji wengine wawili wameuwawa katika shambulio la anga kusini mwa Afghanistan.

Osman ni mmoja kati ya viongozi wanne wa juu wa kundi la Taliban, na alikuwa akiongoza mapigano kusini mwa nchi hiyo.