1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Majeshi ya NATO yakiri mauaji.

25 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBoc

Majeshi yanayoongozwa na NATO nchini Afghanistan yamekiri kutokea mauaji ya raia, mara hii nchini Pakistan.

Ndege ya jeshi la kimataifa linalosaidia kuweka usalama , ISAF, imeshambulia jengo moja nchini Pakistan wakati wakifukuzana na wapiganaji siku ya Jumamosi.

Wakaazi wamesema watu tisa wameuwawa katika shambulio hilo. Msemaji wa jeshi la ISAF ameeleza masikitiko yake na kukiri kuwa ISAF inapaswa kufanya uratibu mzuri wa operesheni zake pamoja na washirika wake wa Afghanistan.

Siku ya Jumamosi , rais Hamid Karzai amelikosoa jeshi linaloongozwa na Marekani kuhusiana na vifo vya raia ambavyo vimefikia watu 90 katika muda wa wiki moja.

Katika jimbo la kusini la Helmand, mwanajeshi mmoja kutoka Uingereza ameuwawa na wengine wanne wamejeruhiwa na mlipuko wa bomu lililotegwa kando ya barabara.