1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Marekani yaachia ngazi Afghanistan.

5 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5p

NATO imechukua udhibiti wa wanajeshi 12,000 wa Marekani nchini Afghanistan.

Majeshi hayo hapo kabla yalikuwa chini ya uongozi wa jeshi linaloongozwa na Marekani.

Hatua hiyo inafikisha idadi ya wanajeshi wanaotumikia katika jeshi la kimataifa linatoa msaada wa kiusalama kufikia zaidi ya wanajeshi 30,000.

Akizungumza katika sherehe za makabidhiano katika makao makuu ya NATO mjini Kabul , kamanda wa majeshi ya NATO nchini Afghanistan Jenerali David Richards, amesema kuwa kuongezwa kwa wanajeshi wa Marekani kutasaidia kulifanya jeshi la ISAF kufanyakazi vizuri zaidi.

Wanajeshi wengine 8,000 wa jeshi la Marekani walioko mashariki mwa nchi hiyo watabaki chini ya uongozi wa Marekani. Ujerumani inawajeshi karibu 2,800 kaskazini mwa Afghanistan.