1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Mateka waachiwa huru.

29 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC67

Wafanyakazi wa kutoa misaada wa Ufaransa waliokuwa wakishikiliwa mateka na kundi la Taliban nchini Afghanistan kwa zaidi ya wiki tatu wameachiliwa huru.

Akizungumza katika ubalozi wa Ufaransa mjini Kabul , mwanamke, ambaye ametambuliwa tu kwa jina lake la kwanza la Celine, amewashukuru wateka nyara wake kwa kuwatendea vizuri na kumheshimu.

Pia amewaomba taleban kumwacha huru mwanamume mmoja raia wa Ufaransa pamoja na raia watatu wa Afghanistan kutoka katika shirika hilo la kutoa misaada la Terre d’Enfance ambao bado wanashikiliwa.