1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL : Mripuko wauwa 27

10 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBk8

Shambulio la kujitolea muhamga maisha kwa kujiripua dhidi ya wanajeshi wa Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO waliokuwa katika doria kwenye soko lililofurika watu kusini mwa Afghanistan limeuwa watu 17 na kujeruhi 30 wakiwemo wanajeshi saba wa mataifa ya magharibi.

Msemaji wa jeshi amesema watoto ni miongoni mwa waliojeruhiwa.

Shambulio hilo limetokea kwenye jimbo la Uruzgan mojawapo ya maeneo yenye vurugu kubwa nchini Afghanistan na ni kitovu cha jimbo lenye kuotesha kasumba.