1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL : Msemaji wa Taliban mbaroni

27 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMD

Msemaji mkuu wa kundi la itikadi kali la Kiislam la Taliban amekamatwa kusini mwa Afghanistan.

Wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan imeripoti kwamba Qari Yousef Ahmadi na kaka yake wametiwa kizuizini hapo jana kufuatia msako wa polisi kwenye jimbo la Helmand ambalo kwa kiasi fulani linadhibitiwa na Taliban.

Ahmadi ni msemaji wa tatu wa Taliban kukamatwa tokea mwaka 2001 na ambaye waandishi wengi wa habari humfuata kwa habari za matumizi ya nguvu na utekaji nyara wa kundi hilo nchini Afghanistan.