1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Mshambulizi ni adui wa binadamu wote

29 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLe

Bomu lililoripuliwa ndani ya basi lililojaa wanajeshi katika mji mkuu wa Afghanistan,Kabul limeua hadi watu 30 na wengine darzeni kadhaa wamejeruhiwa.Baadhi kubwa ya wahanga hao ni wanajeshi waliokuwa wakisafirishwa kwa basi kwenda kazini.Maafisa wa wizara ya ulinzi wamesema,mripuko huo ulisababishwa na mshambulizi aliejitolea maisha muhanga.Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amelaani vikali shambulizi hilo. Amesema,mtu anaejiita Muislamu asingeripua watu wasio na hatia katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.Wanamgambo wa Taliban wamedai kuwa wao ndio waliohusika na shambulizi hilo.