1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL : NATO yachunguza vifo vya raia

23 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpH

Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO umesema inachunguza repoti kwamba raia 25 wameuwawa pamoja na waasi 30 wa kundi la Taliban katika shambulio la anga nchini Afghanistan.

Kikosi cha Kimataifa cha Usaidizi wa Usalama ISAF kinachongozwa na NATO kimesema katika taarifa kwamba ina sababu ya kuamini kwamba waasi hao walianzisha uchokozi wa shambulio hilo la anga wakiwa kwenye nyumba mbili katika jimbo la kusini la Helmand.Mkuu wa polisi wa jimbo hilo amesema waasi hao kwanza walivishambulia vikosi vya NATO ambavyo navyo vikajibu mapigo kwa shambulio hilo la anga.

NATO inasema pia inachunguza madai kwamba waasi waliwauwa raia waliokuwemo ndani ya nyumba hizo.