1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Njia pekee ni kuwaachilia wafungwa wa Taliban

29 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdz

Nchini Afghanistan,wanamgambo wa Taliban waliowazuia raia 22 wa Korea ya Kusini wamesema, majadiliano yao pamoja na serikali ya yamemalizika.

Kwa mujibu wa msemaji wa Wataliban, hakuna sababu ya kufanya mazungumzo zaidi.Njia pekee ya kumaliza mgogoro huo ni kuwaachilia huru wafuasi wa Taliban waliofungwa jela.

Wakorea 23 walitekwa nyara katika Wilaya ya Ghazni juma moja na nusu lililopita.Mateka mmoja ameshauliwa.

Kwa upande mwingine,hatima ya mhandisi wa Kijerumani alietekwa nyara siku 11 zilizopita bado haijulikani.Lakini shirika la habari la Ujerumani DPA limesema,kuna maendeleo yaliyopatikana katika majadiliano ya kumuachilia huru mateka huyo wa Kijerumani.