1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Pakistan na Afghanistan kuondoa maficho ya magaidi kwa pamoja.

13 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZh

Rais Pervez Musharraf amesema kuwa Pakistan na Afghanistan zinahitaji kufanyakazi kwa pamoja kuondoa maficho ya magaidi na kuliokoa eneo hilo kutokana na imani kali za Kiislamu.

Rais wa Pakistan alitoa matamshi hayo katika hotuba mbele ya wajumbe 700 wa kikabila mwishoni mwa mkutano wa siku nne wa viongozi wa kikabila na maafisa wa serikali katika mji mkuu wa Afghanistan , Kabul.

Wajumbe wa mabaraza ya kikabila pia wamekubaliana kutafuta muafaka na wanamgambo wa Taliban ambao wako tayari kuitambua serikali ya rais wa Afghanistan Hamid Karzai. Pia wamekubaliana kuwa vita iliyotangazwa na Marekani dhidi ya ugaidi ni lazima iendelee kuwa sehemu ya mkakati wa usalama kwa mataifa yote Afghanistan na Pakistan.