1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Raia wawili wa Afghanistan wauwawa

28 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxP

Raia wawili wa Afghanistan wameuwawa na mwengine mmoja kujerihiwa katika shambulio la bomu lililofanywa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga maisha kaskazini mwa Afghanistan.

Shambulio hilo liliwalenga washauri wa wa polisi ya Afghanistan kutoka Marekani walio katika mji wa kaskazini wa Kundus. Kundi la wanamgambo wa Taliban limesema limefanya shambulio hilo.

Mkoa wa kaskazini mwa Afghanistan ambao zamani ulikuwa mtulivu sasa umekuwa ukishuhudia wimbi la machafuko.

Mnamo tarehe 19 mwezi huu mshambuliaji wa kujitoa mhanga maisha aliwaua wanajeshi watatu wa Ujerumani katika soko moja mjini Kundus. Raia sita wa Afghanistan waliuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kwenye hujuma hiyo.

Sambamba na hayo, jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani nchini Afghanistan limesema wanamgambo wasiopungua 24 wa Taliban wameuwawa katika mkoa wa kusini wa Helmand.

Wanamgambo hao waliuwawa wakati wanajeshi wa muungano wakisaidia na ndege za kivita walipokabiliana na shambulio la waasi wa Taliban dhidi ya msafara wa magari mkoani Helmand.