1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Risasi za vikosi zimeua raia nchini Afghanistan

4 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMU

Ripoti zinasema idadi fulani ya raia wameuawa nchini Afghanistan,baada ya vikosi vya NATO kufyatua risasi kumzuia mshambulizi aliyejitolea muhanga ambae alielekeza gari lake kwenye mlolongo wa magari ya jeshi.Shambulio hilo limetokea katika barabara kuu iliyo kati ya mji wa Jalalabad na mpaka wa Pakistan.Wakati huo huo, majeshi ya shirika la kujihami la magharibi NATO nchini Afghanistan yameripoti kuwa wanajeshi wake 2 wameuawa katika mapambano yaliotokea wilaya ya Helmand,kusini mwa nchi lakini haikutajwa ni raia wa nchi gani.