1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Shambulizi jipya limeua watu 10 Afghanistan

20 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0K

Nchini Afghanistan,shambulio la kujitolea muhanga limeua si chini ya watu 10 na kujeruhi hadi 40 wengine,katika wilaya ya Paktia.Shambulio hilo, limetokea siku moja tu baada ya wanajeshi 3 wa Kijerumani na raia 6 wa Afghanistan kuuawa katika shambulio la mwanamgambo aliejiripua katikati ya soko kwenye mji wa Kundus,kaskazini mwa nchi. Waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Franz-Josef Jung amesema,vikosi vya Ujerumani vitaendelea kufanya kazi zake nchini Afghanistan,licha ya kutokea vifo vya wanajeshi hao.Akaongezea kuwa mashambulio hayatoizuia Ujerumani kutoa msaada kwa serikali na raia wa Afghanistan,kuijenga upya nchi yao.Katika shambulio la hiyo jana,vile vile raia 13 wa Afghanistan,wanajeshi 5 wa Kijerumani na mkalimani wao walijeruhiwa.Waasi wa Taliban wamedai kuwa ndio waliohusika na shambulio hilo.