1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Shambulizi la mwanamgambo limeua Waafghanistani 5

27 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7CI

Mwanamgambo aliejitolea maisha muhanga amejiripua karibu na kituo cha kijeshi,mashariki ya Afghanistan.Wanajeshi 4 na raia 1 wa Afghanistan wameuawa katika shambulizi hilo.Kwa mujibu wa afisa wa kijeshi wa Marekani,mshambulizi huyo alivaa sare ya kijeshi na alikwenda kwenye mlango mkuu wa kuingilia uwanja wa kituo cha kijeshi cha Bermel na akajiripua.Hicho ni kituo cha wanajeshi wa Afghanistan na vikosi vya kimataifa vinavyoongozwa na NATO katika wilaya hiyo,karibu na mpaka wa Pakistan,eneo ambako Marekani inasema wanamgambo wa Kitaliban na wafuasi wa Al-Qaeda wanajikusanya upya.