1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Steinmeier na Harper wamekutana na Karzai

22 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzT

Waziri wa nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier amesisitiza kuwa Ujerumani itaendelea kusaidia kuijenga upya Afghanistan.Alitamka hayo, baada ya kukutana na rais Hamid Karzai wa Afghanistan mjini Kabul.Kwa upande mwingine,rais Karzai alimshukuru Steinmeier kwa msaada unaoendelea kutolewa na Ujerumani.Hapo awali, waziri Steinmeier aliwatembelea wanajeshi wa Kijerumani katika mji wa Kundus,kaskazini mwa Afghanistan.Siku ya Jumamosi,wanajeshi 3 wa Kijerumani na raia 5 wa Afghanistan,waliuawa katika shambulio la kujitolea muhanga katika mji huo.Waziri mkuu wa Kanada Steven Harper pia amefanya ziara ya ghafula nchini Afghanistan na amekutana na rais Karzai.Kanada ina kama wanajeshi 2,500 nchini Afghanistan,wengi wao wakiwa kusini mwa nchi wakipambana na wanamgambo wa Taliban.