1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL : Taliban iko tayari kwa mazungumzo na serikali

4 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcJ

Wanamgambo wa Taliban wanaowashikilia mateka 21 wa Korea Kusini nchini Afghanistan wamesema wako tayari kuwa na mazungumzo ya ana kwa ana na serikali.

Lakini wamesema kwamba watakutana tu katika maeneo yalioko chini ya udhibiti wao.Wanamgambo hao wanadai kuachiliwa kwa wafungwa wa Taliban wanaoshikiliwa na serikali kwa ajili ya kubadilishana na wafanyakazi wa misaada wa Korea Kusini wanaowashikilia mateka.

Maafisa wa Korea Kusini wanaopigania kuachiliwa kwa raia wake hao wamesisitiza kuwa hawako katika nafasi ya kuweza kutimiza madai hayo ya Taliban.Watekaji nyara hao tayari wamewauwa mateka wawili wa Korea.

Wakati huo huo bado hakuna habari juu ya hatima ya muhandisi wa Kijerumani ambaye anashikiliwa mateka nchini Afghanistan na timu ya kidiplomasia inaendelea kupigania kuachiliwa kwake. Mjerumani mwengine ambaye alitekwa nyara na Taliban ameuwawa kwa kupigwa risasi na wateka nyara wake.